Ugeni kutoka Shirika la SANKU
27 Oct, 2025
Ugeni kutoka Shirika la SANKU
Tarehe 17 Oktoba 2025, Mkurungezi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Dkt Germana Leyna, ametembelewa na Rais wa Shirika la SANKU kwa kanda ya Afrika Bw. Mark Ocitti, ambaye amefika wa lengo la kujitambulisha na kufahamu namna TFNC inavyoshirikiana na SANKU katika uekelezaji wa afua mbalimbali za kilishe hususani katika eneo la urutubishaji wa vyakula. Bw. Ocitti ambaye aliongoza na Mkurugenzi wa Shirika la SANKU upande wa Mashirikiano na Serikali na Wadau Afrika Mashariki Bw. Gwao Omari Gwao, walipokelewa na mwenyeji wao Dkt Germana Leyna na kujadili masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za lishe, ikiwemo maeneo ambayo Shirika hilo limeendelea kushirikiana ili kusukuma kwa pamoja gurudumu la utekelezaji wa afua mbambali za kilishe.