27 Oct, 2025
Ujumbe wa wataalamu wa kutoka Chuo Kikuu cha Eduardo Mondlane, Wizara ya Uchumi na Wizara ya Afya kutoka nchini Msumbiji waliokuja nchini kujifunza kupata maarifa juu ya utekelezaji wa mpango wa kuzuia upungufu wa madini joto (USI), imehitimishwa rasmi leo Oktoa 10, 2025.
Wakizungumza wakati wa kikao cha majumuhisho ya ziara hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Taasisi, wajumbe hao wameonesha kuridhishwa na yale waliyojifuza juu ya utekelezaji wa mpango wa kuzuia upungufu wa madini joto (USI).
Pia wameweka makubaliano ya maeneo mbalimbali ya mashirikiano katika program ya USI hususani kwenye tafiti zenye kutumia mbinu bunifu zitakazotekelezwa kwa garama nafuu.
Katika ziara yao ya siku tano, wajumbe hao waliweza kupata fursa ya kutembelea maabara ya Chakula na Lishe ya TFNC kujifunza namna inavyofanya kazi zake katika uchambuzi wa sampuli mbalimbali za vyakula na zile za kibaolojia Walitembelea wazalishaji wa chumvi katika mashamba ya chumvi na viwanda vya kuchakata chumvi, ili kupata uzoefu wa uzalishaji na usindikaji chumvi katika mnyororo wa thamani.
