KITABU CHA MAPISHI YA VIAZI LISHE CHAZINDULIWA RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI 2026
20 Oct, 2026
KITABU CHA MAPISHI YA VIAZI LISHE CHAZINDULIWA RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI 2026

Kitabu cha "Mapishi ya Viazi Lishe", kilichoandaliwa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zebra Media (ZM), Better Market for Crops Company (BMC) na Serena Hotel - DSM, kimezinduliwa rasmi leo, Oktoba 15, 2026, mkoani Tanga.


Kitabu hicho pamoja na Bango Kitita chake vimezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mheshimiwa Mwanaidi Rajabu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani.


Akielezea mchakato wa maandalizi ya kitabu hicho, Afisa Lishe Mtafiti Mwandamizi kutoka TFNC, Bi. Maria Ngilisho, amesema kitabu hicho kimeandaliwa kwa kushirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwa lengo la kupata mawazo na utaalamu utakaosaidia kuimarisha matumizi ya viazi lishe katika milo ya kila siku ili kuboresha afya.


Amesema Kitabu hicho kinalenga kutoa elimu kwa wazazi, walezi na wananchi kwa ujumla kuhusu namna mbalimbali za kuandaa na kupika viazi lishe ili kuongeza matumizi yake katika kaya na Jamii kwa ujumla ili kuchangia kukabiliana na upungufu wa vitamini A, hususan kwa watoto na wanawake.


Aidha, kwa mujibu wa takwimu zilizotajwa katika maelezo ya uzinduzi, asilimia 33 ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na asilimia 37 ya wanawake wa umri wa uzazi nchini wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitamini A (TDHS 2010), hali inayoonesha umuhimu wa kuimarisha elimu ya lishe na matumizi ya vyakula vyenye virutubisho muhimu ikiwemo matumizi ya viazi lishe


Kwa sasa, kitabu cha "Mapishi ya Viazi Lishe" kinapatikana kupitia tovuti za FAO na TFNC, kwa ajili ya kuwafikia wadau na wananchi wanaotaka kujifunza mapishi ya viazi lishe.