TFNC yawanoa wataalamu wake wa maabara
19 May, 2026
TFNC yawanoa wataalamu wake wa maabara
Mei 18, 2026, Katika jitihada za kuhakikisha kila sampuli inayopimwa inakidhi viwango vya juu vya kimataifa, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imetoa mafunzo ya Usalama wa Maabara na Mipango ya Hatua za Kupata Ithibati (Laboratory Safety and Accreditation Road Map Training ) kwa Wataalamu wake wa Maabara. Mafunzo haya yamejikita katika kuimarisha usalama wa wataalamu wa maabara, usimamizi wa ubora, usahihi wa matokeo, na namna ya kuiandaa Maabara ili kufikia viwango vya ISO — ambavyo ndivyo kipimo cha juu zaidi cha utendaji bora duniani. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika Mkoani Kilimanjaro katika Chuo cha Ushirika Moshi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt.Germana Leyna , amesisitiza umuhimu wa wataalamu haoa kuzingatia mafunzo yanayotolewa kwa umakini mkubwa ili kuleta tija na usahihi katika utendaji wao wa kila siku. Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania ni maabara rejea kwenye ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na kati na Kusini, na matokeo ya uchunguzi wa viashiria vya hali ya lishe na virutubishi yanayotolewa na maabara hii, yanaaminika kimataifa (WHO, CDC, ECSA-HS, IGAD), na kuifanya kuwa maabara pekee ya lishe inayoaminika ukanda huu.