TFNC yatoa mafunzo ya usindikaji Unga kwa watoto wenye umri wa miezi 6 - 24

News Image

Imewekwa: 30th Jun, 2023

Mkurugenzi Idara ya Sayansi ya Chakula na Lishe, Dkt. Analice Kamala akitoa mafunzo kwa vitendo kuhusu athari za sumu kuvu kwa washiriki wa kozi ya muda mfupi ya utengenezaji wa unga mchanganyiko kitaalamu kwa ajili ya watoto wenye umri wa miezi 6-24 inayotolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania hivi karibuni.
Afisa Mtafiti Mwandamizi, Wessy Meghji akitoa maelezo namna ya kuchanganya mazao mbalimbali kwa washiriki wa kozi ya muda mfupi ya utengenezaji wa unga mchanganyiko kitaalamu kwa ajili ya watoto wenye umri wa miezi 6-24 inayotolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania.
Afisa Mtafiti Mwandamizi, Malimi Kitunda akitoa mafunzo kwa vitendo kuhusu njia bora za ukaushaji wa mazao kwa washiriki wa kozi ya muda mfupi ya utengenezaji wa unga mchanganyiko kitaalamu kwa ajili ya watoto wenye umri wa miezi 6-24 inayotolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania.