TFNC yashiriki maadhimisho siku ya maandishi ya nukta nundu

News Image

Imewekwa: 24th Feb, 2024

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imeshiriki katika Kongamano la kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Maandishi ya Wasioona Duniani (Braille) ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Singida kuanzia Februari 20 hadi 22 , 2024

Katika Kongamano hilo Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania imewakilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe Dkt. Esther Nkuba ambapo amebainisha namna wanavyoshirikana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kuwapatia elimu ya lishe watu wasioona kwa kutumia nyenzo rafiki ikiwemo vitabu vya maandishi ya Braille pamoja na redio ndogo zilizorekodiwa sauti za ujumbe wa lishe.

Kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika tarehe 22/02/2024 katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida ambapo Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania inatarajia kutoa Vitabu vyenye ujumbe wa lishe kwa Jumuiya ya Watu Wasioona Tanzania (TBA) zikiwemo zinazohusiana na vijana balehe pamoja na radio zilizoingizwa masomo mbalimbali ya Lishe.