TFNC yapokea wageni kutoka DANISH-NATCOM na UNICEF Tanzania

News Image

Imewekwa: 17th Jan, 2025

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imetembelewa na wageni kutoka Shirika la DANISH- NATCOM, wakiongozana na Maafisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Tanzania, ili kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Taasisi, pamoja na kupata uelewa kuhusiana na masuala ya lishe nchini.

Maafisa hao wamefanya ziara katika Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam na kujionea shughuli zinazotekelezwa na maabara hiyo, ikiwemo upimaji wa sampuli mbalimbali zinazohusiana na vyakula.