TFNC ya shiriki Mkutano wa Kimataifa kuhusu Virutubishi vya Madini na Vitamini nchini Uholanzi

News Image

Imewekwa: 20th Oct, 2023

Tarehe 18 Oktoba,2023 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna, ameshiriki Mkutano wa Kimataifa wa kujadili masuala mbalimbali kuhusu Virutubishi vya Madini na Vitamini unaoendelea kufanyika katika Mji wa The Hague nchini Uholanzi.
Katika Mkutano huo Dkt. Germana ni miongoni mwa wawasilishaji na mwongozaji wa mada inayolenga kujadili umuhimu wa taarifa za Upungufu wa Vitamini na Madini.
Watalaamu wengine kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania watakaoshiriki kwenye Mkutano huo ni pamoja na Dkt. Geofrey Mchau pamoja na Rose Msaki ambao wao watawasilisha taarifa za Utafiti kuhusu Upungufu wa Damu, Madini Joto, na Matibabu ya Utapiamlo Mkali.