TFNC na Global Communities wasaini mkataba wa utekelezaji wa programu ya lishe shuleni

Imewekwa: 17th Mar, 2023
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania pamoja na Shirika lisilo la Kiserikali la "Global Communities" wamesaini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa programu ya Lishe shuleni, itakayohakikisha watoto waliopo shuleni wanakula Chakula kinachokidhi mahitaji yao ya lishe pamoja na kushikirikiana kwenye tafiti za lishe. |
![]() |
Mkataba huo umesainiwa leo Machi 17, 2023 katika Ofisi za Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Dkt. Germana Leyna, pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Global Communities Bw. Nick Ford. Kwa sasa Programu hiyo inatekelezwa katika mikoa ya Dodoma na Mara ambapo mbali na huduma ya chakula kinachotolewa shuleni, wanafunzi, walimu na wazazi watafundishwa kubadili tabia za ulaji,namna ya kutengeneza mlo kamili, ufugaji wa wanyama wadogo wadogo na ulimaji wa bustani. |