TFNC-Kuendelea kushirikia na wadau utekelezaji afua mbalimbali za lishe

News Image

Imewekwa: 21st Jul, 2023

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzani Dkt. Germana Leyna, amesema Taasisi ya Chakula na Lishe itaendelea kushirikiana na wadau katika masuala mbalimbali yanayohusiana na lishe, ili kuweza kutekeleza afua za kilishe kwa pamoja.
Hayo yamebaninishwa Jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao kati ya Mkurungezi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Germana Leyna na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la SANKU Bw. Felix Brooks-Church, kilichofanyika katika Ofisi za Shirika hilo zilizopo Masaki.
Katika kikao hicho, aidha Dkt. Germana alipata wasaa wa kufahamu juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo katika kuimarisha suala la Uongezaji wa virutubisho vya madini na Vitamini katika vyakula, kupitia teknolojia ya mashine zinazofungwa kwenye Mashine za kusanga unga wa Mahindi. “Serikali ipo pamoja nanyi na sisi kama Taasisi tupo tayari kuendelea kushirikiana na kuwapa ushauri wa kitaalamu ili kwa pamoja tuweze kushirikiana katika kuimarisha lishe za Watanzania” alisema Dkt. Germana.
Katika Hatua nyingine Dkt. Germana amewapongeza SANKU kwa jitihada zao wanazochukua katika kusambaza teknolojia yao inayotumika katika urutubishaji wa bidhaa za unga wa mahindi, ambapo amesema zimesaidia kuongeza idadi ya Watanzania wanaotumia unga wenye virutubishi vya madini na Vitamini na kusaidia kupunguza idadi ya wananchi wenye upungufu wa virutubishi hivyo muhimu mwilini.
Hata hivyo kwa upande wake Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la SANKU Bw. Felix Brooks-Church amemuomba Mkurugenzi Mtendaji Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kuendelea kusisitiza juu ya elimu ya umuhimu wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi, suala ambalo Dkt. Germana amesema watashirikiana kwa pamoja ili kuweza kufikia adhma hiyo.