Taarifa za lishe zilizokusanywa kupitia siku ya Afya na Lishe ya Kijiji (SALIKI)

Imewekwa: 6th Mar, 2025
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na mkoa wa Iringa, imekamilisha uchakataji wa taarifa za lishe zilizokusanywa kupitia siku ya Afya na Lishe ya Kijiji (SALIKI) katika halmashauri zote za mkoa huo, taarifa ambazo zitatoa muelekeo wa tatizo la utapiamlo katika ngazi ya halmashauri aidha zitasaidia kupanga mikakati endelevu itakayowezesha kupunguza tatizo la udumavu kwa watoto walio chini ya miaka mitano katila mkoa wa Iringa.
Matokeo ya awali ya viashiria vya lishe yamewasilishwa Machi 5, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna katika kikao maalumu cha kupokea taarifa hizo, kilichoongozwa na Mkuu wa mkoa wa Iringa pamoja na wadau wengine wa lishe.