Semina kwa Watafiti
Imewekwa: 23rd Dec, 2024
Watafiti wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Disemba 20, 2024 wamejengewa uwezo namna ya kutumia taaluma za kilimo, lishe na afya ili kuwawezesha kutumia uhusiano uliopo kati ya Kilimo, Lishe na Afya kukabiliana na magonjwa yatokanayo na changamoto za kilishe.
Mafunzo hayo yamewezeshwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw.Eward Mushi pamoja na Afisa Lishe Mtafiti wa Taasisi ya chakula na Lishe Tanzania Bi. Victoria Kariathi.