Rais wa Shirika la Kimataifa la Nutrition International atembelea TFNC

News Image

Imewekwa: 10th Feb, 2024

Katika ziara hiyo Bw. Joel Spicer ameongozana na jopo la viongozi mbalimbali wa NI wakiwemo wajumbe wa Menejimenti ambao ni Dkt. Mandana Arabi, Margaux Stastny, Asif Nawaz, Grant Carioni, Steve Gilbert, Ann Witteveen, Roushika Gawne, Manoj Kumar and Victor Ogera. Pia wageni hawa waliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la NI Tanzania, Dkt. George Mwita na Mkurugenzi wa Programu ya BRIGHT Tanzania, Dkt. Raphael Katebalila.

Katika ziara hiyo Mr. Spicer alifanya kikao na menejimenti ya Taasisi ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Germana Leyna pamoja na viongozi wengine akiwemo; Mkurugenzi wa Idara ya Afya na Lishe ya Jamii, Dkt. Ray Masumo, Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Chakula na Lishe Dkt. Analice Kamala, Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe Dkt. Ester Nkuba, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Ally Zahoro pamoja na Wakuu wa Vitengo na watafiti.

Katika kikao hicho mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo utekelezaji wa Mpango jumuishi wa kitaifa wa lishe wa pili (NMNAP II) na maeneo ya mashirikiano hususan katika kupambana na lishe duni kwa rika balehe na changamoto za upungufu wa damu kwa kundi hilo na mengine