Programu Ya Kuzuia Upungufu Wa Madini Joto

Imewekwa: 4th Mar, 2023
Mwanasayansi na mtaalamu Mbobezi wa program ya Chumvi (USI) kutoka Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Dkt. Rizwan Yusuf pamoja na wataalamu wengine kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, wamefanya ziara katika halmshauri ya Mkuranga na kukutana na wadau wa chumvi ili kujadili utekelezaji wa programu ya kuzuia upungufu wa madini joto. |
![]() |
Katika ziara hiyo watalaamu hao, pia wamejadiliana juu ya uzalishaji na uchakataji wa Chumvi yenye madini joto na namna ya kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa shughuli za programu hiyo katika halmashauri ya Mkuranga. |
![]() |
Watalaamu hao wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dk. Germana Leyna wamefanikiwa kutembelea mashamba ya wazalishaji Chumvi wa Halmashauri hiyo, na kujionea namna wazalishaji chumvi hao namna wanavyochanganya chumvi na madini joto, kabla ya kuyaingiza sokoni. |
![]() |
Pia timu hiyo ya Wataalamu imetembelea kiwanda cha kuzalisha chumvi cha Neelkhanth Salt Limited kilichopo Mkuranga na kujionea namna shughuli za uzalishaji wa Chumvi yenye madini joto zinazofanyika kiwandani hapo. |