Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya atembelea Maabara ya kupima viini lishe ya TFNC

News Image

Imewekwa: 19th Jun, 2023

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amefanya ziara ya kikazi katika Maabara ya kupima Virutubishi ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania na kuridhishwa na utendaji kazi wa maaabara hiyo katika kupima sampuli mbalimbali za vyakula, zikiwemo sampuli zinazotumika katika tafiti mbalimbali zinazohusiana na masuala ya Chakula na Lishe.

Akizungumza wakati wa ziara yake Naibu katibu Mkuu amesema Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania ina vifaa vya kisasa na ina uwezo wa kuweza kushirikiana na Taasisi nyingine za Serikali katika upimaji wa sampuli mbalimbali zinazohusiana na masuala ya chakula na lishe.