Naibu Katibu Mkuu (Afya)TAMISEMI Dkt. Charles atembelea TFNC

Imewekwa: 25th Aug, 2023
Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Wilson Charles, amekutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, lengo likiwa kufahamu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Taasisi, pamoja na namna wanavyoshirikiana katika utekelezaji wa afua mbalimbali za Lishe. Kikao hicho kimefanyika Agosti 23, 2023 katika Ofisi za Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Jijini Dar es Salaam, ambapo Dkt. Charles ameleeza kuwa Ofisi yake itaendelea kutoa ushirikiano kwa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania ili kuhakikisha masuala ya lishe yanapewa kipaumbele nchini na kuleta matokeo chanya. |