Mwenyekiti wa Bodi ya TFNC akutana na Menejimenti na Watumishi

News Image

Imewekwa: 14th Sep, 2023

Mwenyekiti Bodi ya Usimamizi ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bw. Obey Assery, leo Septemba 14, 2023, amekutana na Menejimenti na Watumishi wa Taasisi na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mikakati ya kuiwezesha Taasisi kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuleta tija kwa Taifa.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt.Germana Leyna, akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji ya Mwaka 2022/23 kwa kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Taasisi (hayupo pichani), wakati wa kikao chake na Menejimenti na Watumishi wa Taasisi, kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na Taasisi.
Katibu wa Wanawake wa RAAWU Tawi la Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bi. Aleswa Swai, akisoma risala ya Wafanyakazi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Taasisi Bw. Obey Assery (hayupo pichani) wakati wa kikao chake na Watumishi wa Taasisi kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali kuhusu Taasisi.
Watumishi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, wakiwa katika kikao cha pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Taasisi Bw.Obey Assery (hayupo pichani) ambapo leo Septemba 14, 2023, anazungumza na Menejimenti na Watumishi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mikakati ya namna ya kuiwezesha Taasisi kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuleta tija kwa taifa.