Mwenyekiti wa Bodi ya TFNC akutana na Menejimenti

News Image

Imewekwa: 31st Aug, 2023

Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bw. Obey Assery, amekutana na Menejimenti ya Taasisi na kujadili masuala mabalimbali ikiwemo kuwapatia mrejesho wa maelekezo yaliyotolewa na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kikao cha Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi Watendaji wa Taasisi kilichofanyika Agosti 19-21, 2023 Jijini Arusha.
Katika Kikao cha Mwenyekiti wa bodi pamoja na Menejimenti ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, wamejadiliana mikakati mbalimbali ya kuiwezesha Taasisi kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuleta tija kwa Taifa.