Mratibu wa Mwongozo wa Chakula na Ulaji akiwa katika mazungumzo na Bw.Zagalo na Bi.Elizabeth kutoka PlateAI Company

News Image

Imewekwa: 19th Feb, 2024

Afisa Lishe Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bi. Maria Ngilisho, ambaye ni Mratibu wa Mwongozo wa Chakula na Ulaji wa Tanzania Bara, akiwa kwenye mazungumzo na Bw. Zagalo Emanuel na Bi. Elizabeth Mmari kutoka "PlateAI Company" miongoni mwa vijana watano ambao kampuni yao lilishinda tuzo na kuweza kuwasilisha ubunifu wao “Application ya simu ya kupanga chakula” katika jukwaa la “Falling Walls Summit” nchini Ujerumani ambapo “Application” hiyo inatajwa itasaidia kutatua matatizo ya Lishe nchini kwa kutumia vyakula vinavyopatikana katika maeneo yetu.

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania imekuwa ikishirikiana na “Plate AI “ kuwapa ushauri wa kitaalam utakaowezesha kuboresha "App" hiyo inayolenga kutatua matatizo ya mwenendo wa ulaji usiofaa kwa kumwezesha mtumiaji kupanga na kuchagua mlo unaokidhi mahitaji ya Lishe yake binafsi kwa kuzingatia Mwongozo wa Chakula na Ulaji.