Mpango Mkakati wa Kisekta wa Lishe Zanzibar 2025-2029

Imewekwa: 17th Jan, 2025
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikichukua juhudi mbali mbali za kuhahakisha huduma ya lishe inaimarika ili wananchi wawe na Afya bora.
Ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Kisekta wa Lishe Zanzibar 2025-2029 uliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar.
Amesema lengo la mpango mkakati huo ni kuimarisha Afya za wananchi na kuondoa changamoto zinazosababishwa na ukosefu wa lishe bora ikiwemo udumavu wa watoto, uzito pungufu na utapiamlo hususan kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano na wanawake wenye umri wa kuzaa ambao ndio walengwa wakubwa wa mpango huo.
Nae Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazurui amesema Ili kuimarisha afya ya mama na mtoto Wizara ya Afya imejipanga kuboresha viashiria vya lishe kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano mama wajawazito na wanafunzi kwa lengo la kutengeneza jamii yenye Afya na lishe bora kwa maendeleo ya Taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto (UNICEF) Tanzania Bibi ELKE WISCH amesema Ukuwaji mzuri wa mtoto unategemea upatikanaji wa lishe bora ambapo tafiti mbali mbali zinaonyesha kuwa asilimia 70% ya watoto nchini hawakuwi vizuri kutokana na kutopatikana kwa lishe bora kwa mama na mtoto.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya zanzibar Dkt Mngereza Mzee Miraji amesema kuwa lishe duni bado ni changamoto kubwa kwa afya ya jamii kwa zanzibar, wakiwemo watoto, vijana na wanawake wenye umri wa kuzaa.
Amesema Wizara ya Afya kwa kishirikiana na Wizara nyengine itahakikisha inatekeleza mpango huo kwa pamoja ili kuondokana na changamoto hizo za lishe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt.Germana Leyna (aliyesimama kulia), Mkurugenzi wa Lishe ,Sera na Mipango Debora Charwe(aliyesimama kushto) pamoja na Afisa Mtafiti Hancy Adam, ni Miongoni wa waalikwa walioshiri kwenye hafla ya uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Kisekta wa Lishe Zanzibar 2025-2029 uliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar.
Mpango huo umezinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ambapo amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikichukua juhudi mbali mbali za kuhahakisha huduma ya lishe inaimarika ili wananchi wawe na Afya bora.
Amesema lengo la mpango mkakati huo ni kuimarisha Afya za wananchi na kuondoa changamoto zinazosababishwa na ukosefu wa lishe bora ikiwemo udumavu wa watoto, uzito pungufu na utapiamlo hususan kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano na wanawake wenye umri wa kuzaa ambao ndio walengwa wakubwa wa mpango huo.