MPANGO KAZI WA UTEKELEZAJI WA MAJUKWAA YA WADAU WA VUGUVUGU LA KUINUA MASUALA YA LISHE NCHINI

Imewekwa: 9th Sep, 2025
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) kwa kushirikiana na shirikila la PANITA leo Agosti 28, 2025, imeandaa kikao kazi cha mashauriano ya pamoja na wawakilishi wa Wizara kuu za Serikali zinazotekeleza Mpango Jumuishi wa Pili wa Taifa wa Lishe (NMNAP II), na wadau wanaounda majukwaa ya vuguvugu la kuinua lishe (SUN Networks), lengo likiwa kuimarisha na kuongeza ushirikishwaji wa majukwaa hayo katika masuala yanayohusu mapambano dhidi ya changamoto za Utapiamlo katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Kikao hicho kilichofanyika Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Zabibu, washiriki wa kikao hicho wamejadili pia mipango ya utekelezaji wa ahadi za nchi zilizoshiriki mkutano wa “4NG 2025” uliofanyika mwezi Machi jijini Paris Ufaransa.