Mkutano wa Uthibitishaji wa Matokeo ya Utafiti kuhusu Gharama ya Utapiamlo Afrika (COHA)

News Image

Imewekwa: 8th Feb, 2025

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Ufuatiliaji wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bwa. Paul Sangawe amefungua Mkutano wa Uthibitishaji wa Matokeo ya Utafiti kuhusu Gharama ya Utapiamlo Afrika (COHA) kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bwa. Sangawe amefungua mkutano huo uliofanyika tarehe 4 Februari 2025 katika ukumbi wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma ambapo amesema lengo la kukutana ni kupitia, kuthibitisha, na kupitisha matokeo na mapendekezo ya utafiti ambao uthibitishaji utakuwa ni jukwaa kwa wadau wakuu wa kitaifa.

Washiriki wa mkutano wa uthibitishwaji wa matokeo ya Utafiti wa Gharama ya utapiamlo Afrika (COHA) kwa pande zote mbili za Muungano (Tanzania Bara na Zanzibar) ulihusisha Wakurugenzi wa Kisekta, Wadau na washiriki wengine Umoja wa Afirika (AUC).

Baadhi ya washiriki hao ni pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Zanzibar), Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu),Wizara ya Afya, Wizara ya Fedha, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Shirika la kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) WFP – AUGO na Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali – Zanzibar, pamoja na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu - Zanzibar