Mkutano wa pili wa Wadau wa masuala ya Urutubishaji vyakula na chumvi wafanyika nchini Kenya

News Image

Imewekwa: 18th Oct, 2024

Mkutano wa pili wa Wadau wa masuala ya Urutubishaji vyakula na chumvi ili kuzuia upungufu wa virutubishi vya madini na vitamin kanda ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, umefanyika Mombasa nchini Kenya katika Hotel ya Sarova Whitesands Beach Reort and Spa, ukilenga kujadili matokeo na mapendekezo ya Mapitio ya Kati ya Program ya Kuzuia Upungufu wa Madini Joto ya mwaka 2022, na kuandaa mpango elekezi na endelevu wa kuzuia upungufu wa madini joto.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna ni miongoni mwa washiriki wa mkutano huo, ambapo pamoja na mambo mengine, umelenga pia kufanya mapitio ya hali ya utekelezaji wa afua ya urutubishaji vyakula na chumvi kwa nchi wanachama wa Kanda ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (ESCA), na kuibua changamoto na fursa zilizopo za kuboresha utekelezaji wa programu ya urutubishaji.

Mkutano huo ulioanza Oktoba 15 hadi 17, 2024, umewakutanisha wataalamu wa masuala ya urutubishaji chumvi na vyakula 102, kutoka nchi 21 zikiwemo zikiwemo Angola, Botswana, Comoros, Democratic Republic of Congo, Ethiopia, Eswatini, Kenya, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Seychelles, Somalia, South Africa, Uganda, United Republic of Tanzania, Zambia and Zimbabwe.

Nchi ya Tanzania iliwakilishwa na wataalamu kutoka Wizara, Taasisi, Wadau wa Maendeleo na Sekta Binafsi kama ifuatavyo: Wizara ya Afya (Mr. Peter Kaswahili), Wizara ya Viwanda na Biashara (Mr. Festo Kapela), TFNC (Dr. Germana Leyna & Ms. Rose Msaki), TBS (Ms. Rhoda Kidolezi), UNICEF (Ms. Joyce Ngegba), Iodine Global Network (Prof.Festo Kavishe, Rosemery Mwaisaka & Dr. Vicent Assey), Nutrition International (Mr. Bernard Makene), na SANKU (Mr. Gwao Gwao).