Mkutano wa 4 wa kimataifa wa lishe kwa maendeleo (Nutrition for Growth- N4G)

Imewekwa: 29th Mar, 2025
Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa Lishe kwa Maendeleo (Nutrition for Growth- N4G) unaofanyika jijini Paris nchini Ufaransa , umeendelea kwa siku ya pili, ambapo katika siku ya hii masuala ya usawa wa upatikanaji wa huduma za lishe kwa wanawake na wasichana yamejadiliwa kwa kina. Pia katika siku hii, wajumbe wa mkutano huuo watajadili uhaba wa baadhi ya taarifa za visababishi na matumizi ya akili mnemba katika kuchataka taarifa za lishe.
Aidha katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt.Germana Leyna, amepata wasaa wa kuwasilisha mada iliyokuwa inajadili uzoefu wa Tanzania katika kupanga na kutekeleza afua muhimu za lishe katika sekta ya afya, mjadala ambao uliandaliwa na World Vision Tanzania na Hellen Keller International ukienda sambamba na Mkutano unaoendelea wa 4NG.
Katika Mkutano huu Tanzania imewakilishwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Ali Jabir Mwadini, Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Uongozi wa Jukwaa la Vuguvugu la Lishe Duniani (Scaling Up Nutrition Movement -SUN) Mhe. Neema Lugangira, Mkurugenzi Msaidizi Uratibu na Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bwa. Omar Ilyas pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania.
Mkutano huo umewakutanisha viongozi wa kiserikali kutoka nchi mbalimbali, mashiriki ya kifedha, benki, Umoja wa Mataifa, NGO za Kimataifa na taifa.
Tanzania imewakilishwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Ali Jabir Mwadini, Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzamia na Mjumbe wa Uongozi wa Jukwaa la Vuguvugu la Lishe Duniani (Scaling Up Nutrition Movement -SUN) Mhe. Neema Lugangira pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Uratibu na Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bwa. Omar Ilyas.