Mkutano Mkuu wa tisa wa wadau wa lishe

News Image

Imewekwa: 26th Oct, 2023

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akitembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ili kujionea utekelezaji wa afua za lishe wakati wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Lishe uliofanyika katika Hotel ya Mount Meru jijini Arusha, ambapo Waziri Mkuu alikuwa mgeni rasmi katika Mkutano huo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezindua rasmi ‘Mashine za Vinyunyizi ambazo zitatumika kuongeza virutubisho kwenye unga wa nafaka unaozalishwa na wasindikaji wadogo nchini, Mashine hizo ambazo zimetengezwa hapa hapa nchini na SIDO chini ya ufadhili wa GAIN kupitia uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) zitasaidia kuendeleza juhudi za pamoja za wadau wa lishe katika kuhakikisha Tanzania inapunguza viwango vya Utapiamlo kwa baadhi ya Viashiria.

Mashine hizo zimenduliwa rasmi wakati wa Mkutano Mkuu wa tisa wa wadau wa Lishe uliofanyika jijini Arusha katika ukumbi wa Mount Meru Hotel.