Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa UN atembelea Maabara ya TFNC

News Image

Imewekwa: 7th Sep, 2023

Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa UN anayeratibu vuguvugu la lishe (Scaling Up Nutrition -SUN) Bi. Afshan Khan akiwa na Wajumbe wengine kutoka Ofisi ya Kanda ya SUN, ametembelea Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania iliyopo Mikocheni Jijini Dar Es Salaam ikiwa sehemu ya ziara ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Maabara hiyo.
Katika ziara hiyo Bi. Afshan Khan ameongozana pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe ambaye pia alipata wasaa wa kumuelezea umuhimu wa Maabara hiyo katika kuchunguza sampuli mbalimbali zinazohusiana na Masuala ya Chakula nchini.
Bi. Khan pamoja na wajumbe wengine wa SUN ni miongoni mwa washiriki wa Mkutano wa AGRF unaoendelea kufanyika nchini kuanzia tarehe 5-8 Septemba 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa JNICC jijini Dar Es Salaam.