Mikakati ya kukabiliana na udumavu mkoa wa njombe

News Image

Imewekwa: 1st Mar, 2024

Februari 27, 2024 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna amepata wasaa wa kushiriki kwenye kikao na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) Mhe. Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na uongozi wa Mkoa wa Njombe ukiongozwa na Mkuu wa mkoa Mhe. Anthony Mtaka, kujadili namna ya Ushirikiano katika kampeni iliyoanzishwa na Mkoa huo katika kuharakisha kasi ya mapambano dhidi ya utapiamlo hususani udumavu na Taasisi ya JMKF.

Utafiti wa kitaifa wa afya ya mama na mtoto na viashiria vya malaria umeonesha hali ya udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano uko 30.4% (Sawa na takribani watoto millioni 3) ambapo Njombe ni miongoni kwa mikoa yenye viwango vya juu Njombe ukiwa na (50%).