Mazungumzo kuhusu maandalizi ya Utafiti wa gharama za utapiamlo nchini yafanyika TFNC

News Image

Imewekwa: 13th Jul, 2023

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germanya Leyna, Julai 10, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Maafisa kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Africa Global Union Office (AUGO), ikiwa ni sehemu ya mwanzo ya maandalizi ya kujadili masuala mbalimbali kwa ajili ya Utafiti kuhusu gharama za utapiamlo nchini.
Utafiti huo unaongozwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) na Shirika la Maendeleo la Umojawa Afrika huku Shirika la Mpango wa Chakula Duniani likipewa jukumu la kutoa msaada wa kitaalamu kwa nchi zinazopanga kufanya utafiti huo. Utafiti huo unafanyika kufuatia makubaliano ya nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kupitia program ijulikanayo kama “The Cost Hunger in Africa- COHA”