Matumizi ya shilingi 1,000 za afua za lishe kwa watoto wadogo zisimamiwe kikamilifu

News Image

Imewekwa: 6th Dec, 2022

Na, Mwandishi wetu Musoma, Mara.

Wabunge vinara wa lishe nchini wameiomba Serikali kuzichukulia hatua halmashauri zinazoshindwa kutenga shilingi 1,000 za afua za lishe kwa ajili ya watoto chini ya umri wa miaka 5, na kuzipa motisha ya kuongeza kiwango hicho cha fedha halmshauri ambazo zimekuwa zikitenga na kufanya vizuri katika matumizi ya fedha hizo ili kuweza kuzisaidia katika utekelezaji wa afua mbalimbali za lishe.

“Halmashauri zinazoshindwa kutenga shilingi 1,000 za afua za lishe kwa watoto wadogo zichukuliwe hatua” Mhe.Esther Matiko mwakilishi wabunge vinara wa lishe nchini katika mkutano mkuu wa wanane wa wadau wa lishe nchini.

Akizungumza wakati wa kilele cha Mkutano mkuu wa nane wa wadau wa lishe nchini uliofanyika Musoma mkoani Mara, mwakilishi wa wabunge hao Mhe. Esther Matiko amesema kuna baadhi ya halmashauri bado zinasua sua katika utengaji wa fedha hizo.

“natambua kuna changamoto hazina kipato toshelezi kutokana na kuwa na bajeti ndogo, hata hivyo bado kuna haja ya kuhakikisha suala hili linasimamiwa na ndiyo maana sisi kama wabunge vinara wa lishe tumekuwa tukishauri zile ambazo zinafanya vizuri tunaomba Serikali kuu iweze kuziongezea kiwango hicho cha fedha.Alisema Mhe.Matiko

Mhe.Matiko amesema mtoto hakidumaa hawezi kuwa na ufahamu wa kuweza kupembua mambo na Taifa haliwezi kuona mchango wake siku za baadae hivyo ni wajibu wa Serikali na Viongozi wengine kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa afua mbalimbali za lishe.

Katika hatua nyingine Mhe.Matiko ameipongeza Serikali katika hatua waliyochukua ya kuendelea kuajiri maafisa lishe katika halmashauri mbalimbali na kuiomba iendelee kuajiri ikiwezekana hadi ngazi ya kata kuwe na maafisa lishe.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika kilele cha mkutano huo ambaye alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mhe.Dkt.Doroth Gwajima ambaye amemwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameigiza OR-TAMISEMI kuhakikisha inasimamia sekretarieti za mikoa kuhakikisha zinatenga fedha hizo na zinatumiwa katika malengo kusudiwa na hatua stahiki ziendelee kuchukuliwa kwa viongozi wataoshindwa kusimamia jambo hilo.

MWISHO