Matokeo ya Utafiti wa majaribio ya Mfumo wa ufuatiliaji wa Takwimu za Chumvi awamu ya Pili

News Image

Imewekwa: 11th Jun, 2025

Wataalamu wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania chini ya Programu ya Kuzuia upungufu wa madini joto pamoja na Wataalamu kutoka Shirika la Iodine Global Network, leo Juni 11 2025, wamekutana jijini Dar es Salaam na kujadili matokeo ya Utafiti wa majaribio ya Mfumo wa ufuatiliaji wa Takwimu za Chumvi (FORTIMAS) awamu ya Pili.

Utafiti huo ambao umefanyika kwa mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Singida na Mtwara na unatajwa utaenda kutafuta njia endelevu na yenye gharama nafuu ya kuweza kutathmini upatikanaji wa madini joto katika kaya na jamii kwa ujumla.

Kwa miaka mingi taifa letu limekuwa likitegemea Utafiti wa Afya ya Mama na mtoto (TDHS) katika kuweza kupata taarifa za upatikanaji wa chumvi yenye madini joto katika jamii yetu, hivyo huu unakuja na njia nyingine rafiki na rahisi yenye gharama nafuu ambayo itaweza kutupa pia taarifa zinazohusiana na madini joto kwa urahisi na zenye usahihi.