Matokeo ya Utafiti kuhusu Gharama ya Utapiamlo Afrika (COHA)

Imewekwa: 29th Mar, 2025
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Henry Kilabuko. Leo Machi 19, 2025 ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara mahsusi zinazohusika kwenye utekelezaji wa Mpango wa Pili Jumuishi wa Masuala ya lishe nchini kujadili na kuidhinisha matokeo ya Utafiti kuhusu Gharama ya Utapiamlo Afrika (COHA) kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bungena Uratibu) jijini Dodoma ambapo amesema lengo la kukutano ni kupitia na kuidhinisha matokeo ya utafiti huo ambao umelenga kubainisha makadirio ya gharama zinazosababishwa na matatizo ya lishe duni/Utapiamlo; Kijamii na kiuchumi na hususani katika nyanja za sekta ya afya, elimu, na nguvu kazi.
Matokeo ya Utafiti huu yatatumika kuongeza uelewa miongoni wa watendaji na watunga sera kuhusu athari za utapiamlo (Katika nyanja za sekta ya afya,elimu na uzalishaji ) kwa kubainisha makadirio ya gharama zake kiuchumi na kijamii.
Aidha, matokeo haya yataongeza chachu katika hatua za kisera ambazo zitachukuliwa ma Serikali kwa misingi ya ushaidi wa kitaalamu kwa lengo la kulinda na kuimarisha rasilimali watu ambayo ndiyo msingi wa ustawi wa taifa letu katika mazingira ya uchumi shindani.