MAFUNZO YA UTEKELEZAJI WA UTAFITI WA FORTIMAS MKOA WA MTWARA

News Image

Imewekwa: 15th Nov, 2024

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Iodine Global Network, Novemba 4, 2024 imetoa mafunzo kwa watendaji wa ngazi ya mkoa na halmashauri ya Mtwara, kuhusu namna watakavyoshiriki kwenye utekelezaji wa utafiti wa programu ya chumvi (USI) unaolenga kuangalia uwezekano wa kutumia mfumo wa afya kupima kiwango cha madini joto katika chumvi na mkojo (USI Surveillance System).



Kukamilika kwa utafiti huu kutaiwezesha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za kwanza Afrika kupima hali ya viwango vya madini joto katika jamii kwa wakati kwa kutumia mifumo endelevu badala ya kusubiri tafiti za kitaifa zinazofanyika kila baada ya miaka mitano. Mikoa mingine inayoshiriki katika utafiti huo ni Singida na Dar es Salaam.