Mafunzo ya Lishe, kozi fupi yakiendelea katika Ukumbi wa TFNC

News Image

Imewekwa: 25th May, 2023

Dkt. Esther Nkuba Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe akifungua mafunzo ya kozi fupi ya namna ya kumsaidia mama kufanikisha unyonyeshaji yanayotolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa wauguzi na wakunga.

Eliasaph Mwana,Mtafiti na Mratibu wa Mafunzo kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania akitoa maelekezo kwa washiriki wa kozi ya muda mfupi ya kumsaidia mama kufanikisha unyonyeshaji inayotolewa na Taasisi hiyo kwa wauguzi na wakunga kwa lengo la kuwajengea uwezo kazini na kufanikisha utoaji bora wa huduma utakaosaidia kutokomeza udumavu kwa watoto

Walbert Mgeni, Afisa Lishe Mtafiti kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania akiwaelekeza jambo washiriki wa kozi ya muda mfupi ya kumsaidia mama kufanikisha unyonyeshaji inayotolewa kwa wauguzi na wakunga kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi