Mafunzo maalum ya matumizi ya mbinu mpya ya MIMI (Modeling and Mapping Risk of Inadequate Micronutrient Intake)
01 May, 2026
Mafunzo maalum ya matumizi ya mbinu mpya ya MIMI (Modeling and Mapping Risk of Inadequate Micronutrient Intake)
Tarehe Aprili 28 2025, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wameanza kutoa mafunzo maalum ya matumizi ya mbinu mpya ya MIMI (Modeling and Mapping Risk of Inadequate Micronutrient Intake) ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za kujenga uwezo wa kitaifa kwa wataalamu katika suala la uchambuzi wa takwimu zinazohusu athari za Viashiria vya upingufu wa Vitamini na Madini Mafunzo haya yatatumika kama fursa ya kimkakati kuimarisha uwezo wa kitaasisi nchini katika kuzalisha ushahidi thabiti unaotokana na takwimu kuhusu upungufu wa vitamini na madini, ili kusaidia katika mikakati ya kuwezesha kufikiwa kwa malengo ya vipaumbele vya maendeleo ya kitaifa kama yalivyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.