MAFUNZO KWA WATAALAMU WA TAKWIMU
Imewekwa: 9th Dec, 2024
Watalaamu wa Takwimu wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na OCGS ni miongoni mwa wataalamu walioshiriki mafunzo ya kujengewa uwezo namna ya kuchambua data ya umasikini wa chakula kwa Mtoto nchini Tanzania.
Mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani Morogoro yamewezeshwa na wataalamu kutoka UNICEF. Wadau wengine walioshirili kwemye mafunzo hayo ni ni pamoja na maafisa kutoka Wizara ya viwanda na biashara, Wizara ya Afya, Wizara ya habari, Wizara ya Maendeleo ya jamii, Wizara ya Kilimo,Wizara ya Elimu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na wengine kutoka Zanzibar.