Mafunzo kwa wadau na wataalamu wa urutubishaji vyakula kutoka maeneo mbalimbali nchini

Imewekwa: 16th Apr, 2025
Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Jamii na Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Ray Masumo, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TFNC wakati wa mafunzo kwa wadau na wataalamu wa urutubishaji vyakula kutoka maeneo mbalimbali nchini yanayofanyika mkoani Morogoro.
Dkt. Ray amesema Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania imekuwa na mchango mkubwa katika kuanzisha, kuendeleza na kukuza ushiriki wa wadau mbalimbali katika utekelezaji wa afua za uongezwaji wa virutubishi kwenye vyakula.
Mafunzo hayo ya siku nne yameandaliwa na Jukwaa la Wadau wa Uongezaji Virutubishi kwenye vyakula nchini (The Tanzania Food Fortification Alliance) (TFFA), Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Afya, Taasisi ya Food Fortification Initiative (FFI), Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania chini ya uwezeshaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF).
Mtaalamu wa lishe Bi Joyce Ngegba kutoka UNICEF, ambaye pia amemwakilisha Msimamizi Mkuu wa Shule za nchini kutoka shirika hilo, akiwasilisha salamu za wadau wa maendeleo, na kuelezea namna shirika hilo la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) walivyo mstari wa mbele katika kufadhili na kuendeleza utekelezaji wa afua za uongezwaji wa virutubishi kwenye chakula.
Mtaalamu wa lishe Bi Joyce Ngegba kutoka UNICEF ameeleza hayo wakati wa mafunzo ya wadau na watalaamu wa urutubishaji vyakula kutoka maeneo mbalimbali nchini yanayoendelea kufanyika mkoani Morogoro.
Mafunzo hayo ya siku nne yameandaliwa na Jukwaa la Wadau wa Uongezaji Virutubishi kwenye vyakula nchini (The Tanzania Food Fortification Alliance) (TFFA), Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Afya, Taasisi ya Food Fortification Initiative (FFI), Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania chini ya uwezeshaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF).
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Chakula na Lishe kutoka TFNC Dkt. Analice Kamala akichangia mada kwenye mafunzo ya wadau na watalaamu wa urutubishaji vyakula kutoka maeneo mbalimbali nchini yanayoendelea kufanyika mkoani Morogoro.
Dkt. Kamala ameelezeahali ya lishe nchini hususani kwenye eneo la upungufu wa vitamin na madini na madhara yake katika afya ya jamii na juhudi zilizochukuliwa na serikali katika kukabiliana na upungufu huo, ikiwa ni pamoja na afua ya kuongeza virutubishi kwenye chakula.
Aidha Dkt. Kamala alielezea jinsi mpango wa urutubishaji chakula ulivyoandaliwa na namna Taasisi ya Chakula na LIshe Tanzania (TFNC) ilivyokuwa mstari wa mbele katika kuanzisha na kuendeleza mpango huo.