Mafunzo elekezi kwa watumishi wapya

Imewekwa: 11th May, 2025
Tarehe 07 Mei, 2025, Mkurugenzi wa Fedha, Utawala na Rasilimali Watu wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Tito Kasambala, amefungua mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya wa Taasisi, ambapo amewataka kutumia Taaluma zao katika kusaidia kutatua changanoto mbalimbali za masuala ya chakula na lishe zinazoikabili jamii.
Bwa. Kasambala amewataka watumishi hao kuzingatia mafunzo wanayopatiwa kwani yatakuja kuwa msingi nzuri wa utekelezaji wa majukumu mbalimbali ndani na nje ya Taasisi.
Kwa mujibu wa waraka namba 5 wa mwaka 2011 wa Utumishi, unaelekeza kila waajiriwa wapya ni lazima wapatiwe mafunzo elekezi ili kuwawezesha kufahamu uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Taasisi husika, pamoja na kufahamu sheria mbalimbali za utumishi na utawala bora.