Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani 2020

News Image

Imewekwa: 29th Nov, 2020

Katika kuelekea siku ya UKIMWI Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Disemba Mosi ya kila mwaka, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania imeendelea kutoa elimu ya Lishe katika viwanja vya Mandela vilivyopo Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro, ambako kunafanyika maonesho mbalimbali ikiwa kuelekea kwenye maadhimisho ya siku hiyo, ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani humo.

Tunapenda kuwakaribisha wote kuweza kutembelea banda letu, ili kuweza kupata elimu zaidi kuhusu masuala ya Chakula na Lishe ikiwemo Lishe sahihi na ulaji unaofaa kwa mtu anayeishi na Virusi vya Ukimwi.