Kikao kuhusu utekelezaji wa shughuli za lishe

News Image

Imewekwa: 4th May, 2025

April 28, 2025, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imetembelewa na wageni kutoka Shirika la Nutrition International wakiongozwa Mkurengezi wa Shiriki hilo nchini Tanzania Dkt. George Mwita, na kujadili masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za lishe, ikiwemo maeneo ambayo Shirika hilo linaweza kushirikiana ili kusukuma kwa pamoja gurudumu la utekelezaji wa afua mbambali za kilishe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna aliongoza kikao hicho akiambatana na Wakuu wa Idara, Wakuu wa Vitengo na sehemu, ambapo amewakaribisha NI kuweza kuungana katika kushirikiana kwenye utekelezaji wa shughuli mbalimbali za lishe.