Kikao kuhusu masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za lishe

Imewekwa: 18th May, 2025
Mei 15, 2025, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imetembelewa na wageni kutoka Shirika la Engender Health Tanzania na kujadili masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za lishe ikiwemo kwenye eneo la Utafiti.
Ugeni huo uliongozwa na Mwakilishi wa Engender Health Tanzania nchini Tanzania, Dkt.Moke Magoma ambaye aliongozana na maafisa wengine kutoka Shirika hilo.