Kikao kazi kulichofanyika TFNC kuimarisha utekelezaji wa Shughuli za Kuzuia Upungufu wa Madini Joto

News Image

Imewekwa: 27th Jun, 2021

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) hivi karibuni walikutana kujadili njia zinazoweza kuimarisha utekelezaji wa Shughuli za Kuzuia Upungufu wa Madini Joto kwa kaya zinazoishi visiwa vya Pemba na Unguja.

Takwimu zinaonesha kuwa Zaidi ya Asilimia 70 ya wananchi wanaoishi katika visiwa vya Unguja na Pemba hawatumii chumvi yenye madini joto ya kutosha, hivyo kupelekea kuwa kwenye hatari kubwa ya kupata madhara yatokanayo na upungufu wa madini hayo mwilini.

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na wadau imekuwa ikisisitiza matumizi ya Chumvi yenye madini joto, hata hivyo mpaka sasa ni asilimia 62 ya Watanzania wanatumia chumvi yenye madini joto, na lengo ni kuhakikisha wanafikia asilimia 90.