KIKAO KAZI KUJADILI MATOKEO MRADI WA IMAN

News Image

Imewekwa: 14th Dec, 2024

Novemba 13, 2024 Wajumbe wa Kamati ya Ushauri wa Kitaalamu ya kusimamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha lishe ya wanawake wajawazito (IMAN) uliotekelezwa mkoani Mbeya, wamekutana jijini Dodoma na kujadili masuala mbalimbali kuhusiana na matokeo ya utafiti wa mradi huo. Sambamba na hilo wajumbe hao wamejadili hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa katika kuhakikisha lishe ya wanawake wajazito inaboreshwa zaidi nchini kutokana na matokeo yaliyopatikana kupitia tafiti hiyo.

Mkurugenzi wa Huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya Dkt. Ahmad Makuwani, akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wajumbe wa Kamati ya Ushauri wa kitaalamu ya kusimamia utekelezaji wa mradi wa kuboresha lishe ya wanawake wajawazito (IMAN), kilichofanyika leo Novemba 13, 2024 jijini Dodoma kikillenga kujadili masuala mbalimbali kuhusiana na matokeo ya utafiti wa mradi huo.

Sambamba na hilo wajumbe hao wamejadili hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa katika kuhakikisha lishe ya wanawake wajazito inaboreshwa zaidi nchini kutokana na matokeo yaliyopatikana kupitia tafiti hiyo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt.Germana Leyna, akibainisha namna Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na Wadau wengine, namna walivyoshiriki kusimamia na kutekeleza mradi wa kuboresha lishe ya wanawake wajawazito (IMAN) uliotekelezwa mkoani Mbeya.

Msimamizi Mkuu wa Shughuli za lishe nchini kutoka UNICEF Bw. Patrick Codjie, akibainisha namna walivyoshiriki katika utekelezaji wa mradi wa kuboresha lishe ya wanawake wajawazito (IMAN) mkoani Mbeya.

Kikao hicho kimewakutanisha wajumbe mbalimbali ikiwemo kutoka Wizara ya Afya, OR TAMISEMI, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, UNICEF, IHI, MUHAS, COUNSENUTH, HKI, R4D, JHPIEGO na RMO mkoa wa Mbeya ambaye aliambatana na ya Maafisa Lishe.

Mradi wa IMAN ulikuwa ukitekelezwa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na wadau wengine, chini ya ufadhili wa UNICEF.