01 May, 2026
Tarehe 22/04/2026, Uongozi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) umekutana na timu ya wataalamu kutoka Uchumi Institute kwa ajili ya kikao kazi cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango Mkakati (Strategic Plan) unaomaliza muda wake, na kuanza maandalizi ya kuandaa Mpango Mkakati mpya.
Tathmini hii ni hatua muhimu katika kupima mafanikio tuliyofikia, kutambua changamoto, na kuweka mikakati thabiti ya kuendeleza mapambano dhidi ya utapiamlo na kuimarisha afya ya jamii nchini.
