Kikao kazi cha kuandaa Mwongozo wa utoaji elimu ya lishe cha fanyika mkoani Mbeya

News Image

Imewekwa: 21st Jul, 2023

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe Wizara ya Afya, Neema Joshua akielezea kwa ufupi malengo ya kikao kazi cha kuandaa Mwongozo wa utoaji elimu ya lishe utakaotumiwa na viongozi wa dini Tanzania Bara.
Afisa Lishe Mtafiti kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Fatma Mwasora akiwasilisha mada kuhusu lishe ya mjamzito na mama anayenyonyesha wakati wa kikao kazi cha kuandaa Mwongozo wa utoaji elimu ya lishe utakaotumiwa na viongozi wa dini Tanzania Bara. Kikao hiki kinachofanyika katika ukumbi wa Usungilo jijini Mbeya. Kikao hiki kimeandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la @helvetas_tanzania ambapo kimeudhuriwa na wadau na wataalamu wa lishe na Mawasiliano kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI, wadau wa maendeleo pamoja na viongozi wa dini. pamoja na World Vision, Save the Children, CRS na Action Against Hunger