Kikao cha Uongozi wa Jukwaa la Vuguvugu la Lishe Duniani na wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya (EU)

Imewekwa: 29th Mar, 2025
Mjumbe wa Uongozi wa Jukwaa la Vuguvugu la Lishe Duniani (Scaling up Nutrition Movement - SUN) ambaye pia ni Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Neema Lugangira ameshiriki vikao na wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) na Bunge la Uingereza pembezoni mwa Mkutano wa Kimataifa wa Lishe na Maendeleo (Nutrition for Growth Summit-N4G) unaoendelea Jijini Paris nchini Ufaransa.
Kikao hicho kimebebwa na agenda kuhusiana na - Ufadhili wa masuala ya lishe kwa nchi zinazoendelea, kwa kuzingatia zaidi Tanzania + kwa kuzingatia hali ya sasa ya misaada ya maendeleo.
Mhe.Lugangira ni miongoni mwa viongozi wanaoshiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Lishe na Maendeleo (Nutrition for Growth Summit-N4G) unaoendelea Jijini Paris nchini Ufaransa.