KIKAO CHA TATHMINI MASUALA YA LISHE (MTR)
27 Oct, 2025
KIKAO CHA TATHMINI MASUALA YA LISHE (MTR)
Wawakilishi kutoka Wizara za Serikali, Idara na Wakala (MDAs), Washirika wa Maendelea, Asasi za Kiraia, Vyuo vikuu, Sekta binafsi pamoja na wadau wengine wa masuala ya lishe, leo Oktoba 23 2025, wamekutana jijini Dodoma kujadili matokeo ya tathimini ya kati (MTR) ili kusaidia kutoa muelekeo wa baadae wa mambo muhimu ya kuzingatia katika maandalizi ya mpango Jumuishi wa Kitaifa wa Masuala ya Lishe (NMNAP III) kwa kipindi kingine cha miaka mitano inayofuata. Akifungua kikao hicho Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bung na Uratibu) Bw. Omar Ilyas amesema tathmini ya muda wa kati (MTR) imefanyika kwa lengo la kupima maendeleo yaliyofikiwa, kubaini upungufu, kutoa mapendekezo ya kuimarisha utekelezaji wa mpango kwa kipindi kilichobaki na Tathmini hii itasaidia pia kutoa taarifa ya mambo muhimu ya kuzingatia katika maandalizi ya mpango mwingine yaani NMNAP III. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Mipango ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Bi Debora Charwe ambaye pia amemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TFNC katika kikao hicho, amewaomba wadau walioshiriki kwenye tathimini hiyo, kushiriki kikamilifu katika kuboresha MTR hii kwani kwa kufanya hivyo kutaisaidia kuandaa njia nzuri katika uandaaji wa Mpango Jumuishi wa masuala ya lishe ujao. Serikali kwa kushirikiana na wadau, inaendelea kutekeleza Mpango Jumuishi wa Pili wa Taifa wa masuala ya Lishe tangu Julai 2021/202 na ili kuhakikisha uwajibikaji na hatua za kisera zinazotegemea ushahidi wa kisanyansi zinaendelea kuchukuliwa, tathmini ya muda wa kati (MTR) imefanyika kwa lengo la kupima maendeleo yaliyofikiwa, kubaini upungufu, kutoa mapendekezo ya kuimarisha utekelezaji wa mpango kwa kipindi kilichobaki na Tathmini hii itasaidia pia kutoa taarifa ya mambo muhimu ya kuzingatia katika maandalizi ya mpango mwingine wa miaka mitano unaofuata.