Kikao cha majadiliano Mradi wa IMAN

Imewekwa: 4th May, 2025
April 28, 2025, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imetembelewa na wageni kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) na kujadili masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za lishe ikiwemo mradi wa IMAN.
Ugeni huo uliongozwa na Msimamizi Mkuu wa Shughuli za Lishe nchini kutoka UNICEF Bwa. Patrick Codjia ambaye aliongozana na maafisa wengine kutoka Shirika hilo.