Kikao cha maandalizi kuelekea Mkutano Mkuu wa Wadau wa Lishe kwa mwaka 2025

News Image

Imewekwa: 16th Apr, 2025

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna kwa lengo la kujadili maandalizi ya kuelekea Mkutano Mkuu wa Wadau wa Lishe kwa mwaka 2025 ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Agosti, 2025.

Kikao hicho kilifanyika tarehe 14 Aprili, 2025 katika ofisi yake Jijini Dodoma, ambapo Katibu Mkuu ameutaka uongozi wa Taasisi hiyo kushirikiana na Ofisi yake kuandaa mkutano huo kwa viwango vya juu ili uendelee kuleta tija kwa Taifa na mafanikio makubwa kama inavyokusudiwa.

Kikao hicho kimeudhuriwa na baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Bw. Paul Sangawe, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi hiyo, Bw. Augustino Tendwa, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bw. Eniud Mbuge, Mratibu wa Masuala ya Lishe Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Abigael Marwa, Bi Hawa Mpunji kutoka Wizara ya Afya pamoja na watendaji wengine kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania.