Kikao cha kujadili njia shirikishi kwa wataalamu wa afya kuhudhuria kozi za muda mfupi

News Image

Imewekwa: 25th Aug, 2024

Tarehe 22, Agosti 2024 Wabobezi wa fani ya HCD (Human Centered Design Approach) kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), wamekutana Kibaha mkoani Pwani kujadili njia shirikishi za kutatua changamoto zinazochangia waalaamu wa afya kushindwa kuhudhuria kozi za muda mfupi zinazohusiana na masuala ya Chakula na Lishe Lishe.

Pia watalaamu hao watajadili na kutengeneza njia sahihi za kuwafanya wanaoudhuria mafunzo hayo waweze kutumia ujuzi wanaoupata katika kuwasaidia Watanzania na kuleta tija kwa taifa.