Jukwaaa la Pamoja la Taarifa na Takwimu za Lishe Nchini sasa lazinduliwa rasmi.

News Image

Imewekwa: 17th Dec, 2020

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza na watendaji wa Serikali ambao wanatakiwa kusimamia jukwaa la pamoja la taarifa na takwimu za lishe nchini (hawapo pichani) namna ambavyo wanaweze kuendesha jukwaa hilo, ambapo amewataka kuwa makini na matumizi ya takwimu hizo zitakazoingizwa kwenye mfumo huo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akibofya kitufe katika kompyuta mpakato kuashiria uzinduzi rasmi wa Jukwaa la Pamoja la taarifa na takwimu za Lishe Nchini, Uzinduzi huo umefanyika jijini Dodoma Disemba 17, 2020 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, aliyesimama kushoto kushuhudia uzinduzi huo ni Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi na kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt Germana Leyna.